Wizara ya Viwanda na Biashara imeandaa Mikutano ya kibiashara ya wadau wa ndani na nje ya nchi itakayofanyika kwa njia ya mtandao ili kutoa fursa kwa wafanyabiashara kutangaza biashara zao kimataifa kupitia maonyesho ya mwaka huu ya sabasaba huku kauli mbiu ikiwa ni “Uchumi wa Viwanda kwa ajira na viwanda endelevu”.

Akizungumza na waandishi wa habari Waziri Viwanda na Biashara, Kitila Mkumbo amesema kuwa maonyesho ya mwaka huu yameboreshwa kwa kuwekwa kwa mitaa maalumu ya kibiashara ikiwemo mtaa wa kilimo, mtaa wa Madini na Mtaa wa wajasiriamali na viwanda vidogo vidogo.

Aidha Waziri Mkumbo ameziasa mamlaka za Serikali za Mitaa, Wakuu wa Mikoa, wakurugenzi wa Halmashauri , Wakuu wa Wilaya na Madiwani kuwahimiza wajasiriamali wa maeneo ya kushiriki.

Sambamba na hayo Mwaka huu pia kutakuwa na kibanda maalum kwa ajili ya walemavu ambalo litatoa fursa ya walemavu kushiriki maonyesho na kupata fursa ya kutangaza bidhaa zao kitaifa na kimataifa.

Maonyesho ya mwaka huu ni ya 45 ambapo zitashiriki nchi saba, makampuni ya nje ya nchi 51 na makampuni ya ndani ya nchi ni 2803 na kwa mwaka huu maonesho hayo yataanza Juni 28, mpaka Julai 13.

Tatueni kero za jamii- Naibu Waziri wa Afya
Marekani yapitisha sheria ya dharura bomba la mafuta