Nchi za Afrika zimeanza rasmi kufanya biashara chini ya eneo huria la kibiashara kote barani humo baada ya miezi kadhaa ya ajizi iliyosababishwa na janga la virusi vya corona.

Eneo hilo la biashara huria la Afrika linalenga kuwaleta pamoja watu bilioni 1.3 katika uchumi wa dola trilioni 3.4, hilo likiwa ndilo eneo kubwa la kibiashara tangu kuundwa kwa Shirika la Biashara Duniani WTO.

Wanaoliunga mkono eneo hilo wanasema litainua biashara miongoni mwa nchi jirani za Afrika.

Benki ya Dunia inakadiria kwamba eneo hilo huenda likawatoa mamilioni ya watu kutoka kwenye umaskini ifikiapo mwaka 2035.

Biashara katika eneo hilo ilikuwa inatarajiwa kuzinduliwa mnamo Julai mosi ila uzinduzi huo ukaahirishwa kwa kuwa mazungumzo ya wahusika ya moja kwa moja hayakuweza kufanyika kutokana na janga la virusi vya corona.

Bunge la seneti Marekani laishinda turufu ya Trump
TRA yavunja rekodi ya makusanyo