Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu wametaka kufutwa kwa uamuzi wa Rais Donald Trump kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.

Mawaziri hao waliokutana mjini Cairo, Misri, katika mkutano wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu wameuita uamuzi wa Trump kuwa ni hatua hatari.

Aidha, mawaziri hao pia wamelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio la kuulaani uamuzi wa Trump, ingawa wamekiri kuwa kuna uwezekano mkubwa wa azimio hilo kupigiwa kura ya turufu na Marekani.

Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina, Riyad Al-Maliki, amesema kuwa endapo Marekani italipigia kura ya turufu azimio hilo, mataifa ya Kiarabu yatasaka azimio jingine kupitia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Zitto aonyesha kutoridhishwa na maamuzi ya JPM
LHRC champongeza JPM