Kiungo mshambuliaji hatari wa Plateau United Isah Ndala, amesema wanakuja Tanzania kuishangaza dunia, kwa kupindua matokeo dhidi ya Simba SC na kisha kusonge mbele kwenye hatua inayofuata ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ndala ametangaza vita hiyo dhidi ya Simba dakika chache kabla ya kuanza safari nchini Nigeria kuja Dar es salaam, tayari kwa mchezo wa mkondo wa pili utakaochezwa Jumamosi (Desemba 05) Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Ndala ambaye hakufurahishwa na matokeo dhidi ya Simba Jumapili (Novemba 29), kabla ya kutoa tambo hizo aliwaomba radhi mashabiki wa Plateau United kwa kupoteza mchezo huo.

“Hii si jinsi tulivyotazamia mchezo huu uwe, bali kwenye soka ni lazima tukubali kwa matokeo yoyote yanayokuja upande wetu.”

Kuhusu Wanigeria kuwatoa Plateau United, Ndala amesema safari ya Dar-es-Salaam itakuwa njema na yenye matumaini makubwa, lakini akaongeza kuwa wadau wa soka nchini humo hawapaswi kuitoa timu yao kwa sababu bado kuna mchezo wa marudiano.

“Simba imekuja Nigeria na kupata ushindi, pia tutasafiri kwenda Tanzania kuionyesha dunia tunauwezo wa kushinda popote,” amesema kiungo huyo kinda.

Akiwa ana hakika kuwa timu yake itashinda jijini Dar-es-Salaam, kiungo huyo alihitimisha na “Msiiweke kando Plateau United.”

Plateau United itahitaji ushindi wa mabao 2-0 ama zaidi ili kusonga mbele wakati timu hizo zitakaporudiana Jumamosi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam majira ya saa 11 jioni, wakati Simba yenyewe itakuwa ikihitaji sare ya aina yoyote au ushindi.

Mshindi wa jumla kati ya Simba na Plateua United, atakutana na Costa do Sol ya Msumbuji ama FC Platinum ya Zimbabwe ambayo katika mechi ya awali nayo ilishinda kwa mabao 2-1 ugenini.

Uingereza kuanza kutoa chanjo ya Covid-19 wiki ijayo
Wahitimu darasa la 7 kuripoti shule kila wiki

Comments

comments