Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako , ameagiza tume ya vyuo vikuu TCU na Baraza la Vyuo vya ufundi (Nacte) kufanya mapitio ya nyezo wanazotumia kukagulia ubora wa vyuo na kuvikagua na endapo vitabainika havijakidhi ubora ameamuru vyuo hivyo kufungiwa mara moja hata kama ni vya serikali.
Hayo yamezungumzwa bungeni pindi alipokuwa akijibu hoja za wabunge waliochangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya wizara ya Elimu kwa mwaka 2018/2019.
”Nacte na TCU wamekuwa wakivifungia vyuo vingi lakini tatizo bado lipo, kwa hiy naviagiza vyombo vya udhibiti wa elimu kufanya mapitio upya ya nyezo za ukaguzi ikiwamo sifa za walimu, mitihani inayotolewa na usahihishaji wao,” amsema Ndalichako.
Ameongezea kuwa” iwapo watabaini havikidhi ubora wavifungie bila kuogopa mtu yeyote hata kama vikiwa vya Serikali vifungieni,”.
Aidha amewataka maofisa Elimu kusimamia kwa ukaribu ubora wa elimu katika shule zilizopo maeneo yao.