Kufuatia mazishi ya mwanafunzi Akwilina Akwiline aliyezaliwa Aprili 1, 1996 na kufariki dunia Februari 16, 2018 kwa kupigwa risasi ya kichwani akiwa kwenye daladala akielekea Bagamoyo kufuatilia eneo la kufanyia mafunzo kwa vitendo ”Field”.
Mwanafunzi huyo ambaye alikuwa akisoma mwaka wa kwanza katika chuo kikuu cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), amekuwa akifadhiliwa na Bodi ya Mkopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB).
Kupitia fedha za mkopo alizokuwa akifadhiliwa na serikali ili kujikimu na maisha ”Boom” Akwilina alikuwa akimsomesha mdogo wake wa kike aliyejulikana kwa jina la Angelina ambaye kwa sasa yupo kidato cha tatu.
Hivyo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akiwa kama kiongozi wa serikali aliyeongoza mazishi hayo tangu msiba ulipotokea mpaka siku ya leo ya mazishi, amepata taarifa juu ya majukumu aliyokuwa nayo marehemu Akwiline kwa mdogo wake.
-
Video: Chadema wasingeandamana Akwilina asingefariki dunia – Kubenea
-
Makonda akemea kunyosheana vidole shambulio la Akwilina, aagiza kupisha uchunguzi
Hivyo kupitia nafasi yake ameahidi kuchukua jukumu la kumsomesha mdogo wa Akwilina mpaka pale atakapomaliza masomo yake na kuanza kujitegemea.
”Nimesikitika pia kuona kwamba pamoja na fedha zile ambazo akwilina alikuwa anapata kwa ajili ya yeye kujikimu lakini alikuwa anatumia fedha hizo hizo kumsaidia mdogo wake Angela ambaye yupo kidato cha tatu”
Ameongezea ”Naomba nisema kwamba huyo binti Angela nitamchukua kwa sababu ninatambua nakuthamini elimu nitahakikisha kwamba nitamsomesha mpaka pale uwezo wake na upeo wake utakapo fikia”
Aidha amewaomba watu wote waungane katika msiba kudumisha amani na upendo.