Waziri wa elimu Sayansi na Technologia. Professa Joyce Ndalichako amewaonya maafisa elimu wa mikoa wanaomdanganya Rais kuwa wamemaiza tatizo la upungufu wa madarasa.
Amesema maofisa hao wanaongeza idadi ya wanafunzi katika shule za zamani na kusababisha wanafunzi hao kufanya vibaya katika mitihani yao ya mwisho.
Professa Ndalichako ametoa onyo hilo alipotembelea ukaguzi wa ukarabati katika shule ya sekondari Kilimo ya Kilosa mkoani Morogoro amabyo inakarabatiwa kwa sh. 752, 094, 254 amabzo ni kutoka serikali kuu.
Alisema ameamua kutoa onyo hilo katika kipindi hiki cha matokeo ya darasa la saba yameshatoka na hivi sasa maofisa hao wapo katika haua ya kuwapangia shule wanafunzi wanaotakiwa kuanza kidatocha kwanza mwakani.
Aidha amesema Rais John Magafuli amekuwa akifanya jitihada za kukusanya kodi na kama kuna upungufu wa madarasa ana uwezo mkubwa wa kumaliza tatizo hilo kwa kuwa amedhamiria kutoa elimu bure.
Katika hatua nyingine mkuu wa wilaya ya Kilosa, Adam Mgoy amesema kuwa mafanikio ya ukarabati huo yametokana na ofisi yake kusimamia kwa karibu zaidi ili kuhakikisha fedha hizo zinatumika vizuri na kuleta tija katika elimu.
Naye kuu wa shule hiyo Mbaraka kupela ameishukuru serikali kwa kuipatia fedha shule hiyo kwaajili ya ukarabati amabo kwa sasa umefikia asilimia 75.