Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako amesema kuwa atautumia muda wake wa mapumziko leo kuhakikisha anaandaa ratiba ya mitihani ya taifa ya Darasa la nne, la saba na kidato cha nne mara baada ya Rais Dkt. John Magufuli kuamuru kufunguliwa shule zote nchini ifikapo Juni 29, 2020.
Kwa mujibu wa kituo cha habari cha Azam Tv, Ndalichako amesema uamuzi uliochukuliwa na Rais Magufuli ulikuwa unasubiliwa kwa hamu na wizara yake.
“Hapa nikitoka saizi sitalala hadi nihakikishe nimetengeneza ratiba ya mitihani darasa la saba, kidato cha nne na darasa la nne, huu uamuzi nilikuwa nausubiri kwa hamu”amesema.
Ikumbukwe kuwa Rais Magufuli mapema leo, wakati akihutubia Bunge, ameagiza shule zote kufunguliwa rasmi kutokana na kupungua kwa maambukizi ya virusi vya Corona nchini.