Mambo si mazuri kwa Mbeya City ambayo imeangushwa kwa kutwangwa mabao 4-1 na wenyeji wake Ndanda FC.
Ndanda FC iliyokuwa nyumbani Nangwanda Sijaona imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao hayo katika mechi ya Ligi Kuu Bara.
Ndanda FC iliyoitoa jasho Yanga katika mechi iliyopita licha ya kupoteza kwa bao 1-0, leo ilionyesha soka safi na la kuvutia na kuonyesha kuwazidi wageni wake katika kila idara.
Wakati Mbeya City ikiangukia pua, Azam FC imefanikiwa kuwaangusha Mgambo FC wakiwa kwao kwenye Uwanja wa Mkwakwaji mjini Tanga.
Mechi hiyo ilikuwa ngumu na yenye kasi licha ya kuchezwa kwenye Uwanja mbovu kabisa wa Mkwakwani.
Stand United ikiwa nyumbani Kambarage katika mji wa madini mengi zaidi nchini wa Shinyanga imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya jirani zao, Toto African.
MATOKEO:
Simba 2-0 JKT Ruvu
Mgambo 1-2 Azam
Ndanda FC 4-1 Mbeya City
Stand United 2-1 Toto
Prisons 2-1 Coastal

Bifu Jipya: Rick Ross amchana Birdman kuhusu Lil Wayne
Maafande Watuma Salamu Kwa Ndugu Zao Wa Mbeya