Watu kumi na watano wamepoteza maisha na mmoja amenusurika baada ya ndege ya mizigo ya Iran aina ya Boeing 707 kuanguka saa chache zilizopita.
Ndege hiyo imeanguka ilipokuwa ikijaribu kutua katika Uwanja wa Ndege wa Fath ulioko Kilometa 40 kutoka Tehran, unaomilikiwa na Jeshi la Mapinduzi la nchi hiyo.
Jeshi hilo limeeleza kuwa ndege hiyo iligonga ukuta na kuanguka baada ya kumshinda rubani. Imeelezwa kuwa mtu pekee aliyekutwa akiwa hai kati ya watu 16 ni mhandisi wa ndege.
Kisanduku maalum cha kutunza kumbukumbu za taarifa za ndege (black box) kimepatikana katika eneo la tukio, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iran.
-
Mahakama yapiga chini shauri la kupinga Muswada wa Vyama vya Siasa
-
Wananchi Ludewa wachimba Barabara kwa mikono
Ndege hiyo ya mizigo ilikuwa ikisafirisha nyama kutoka jiji la Bishkek nchini Kyrgyz. Serikali imeeleza kuwa watu wote waliopoteza maisha kutokana na ajali hiyo ni raia wa Iran.
Chanzo: BBC