Ndege mmoja amesababisha safari ya Ndege ya Kampuni ya Air Asia X iliyokuwa ikitokea nchini Australia kuelekea Kuala Lumpur inchini Malaysia kuahirishwa safari mara baada ya ndege huyo kuanza kutoa milio ndani ya ndege hiyo.
Aidha, abiria waliingiwa na hofu kubwa na kutoa ripoti hiyo ya milio tofauti tofauti ya ndege ndani ya ndege hiyo ya Air Asia X kitu ambacho kilisababisha kutua kwa dharula katika uwanja wa ndege wa Brisbane nchini Australia.
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Benyamin Ismail amesema kuwa rubani wa ndege hiyo na wafanyakazi waliamua kuchukua hatua hiyo ili kuweza kuwahakikishia usalama abiria ambao walikuwa wamejawa hofu.
Hata hivyo, Ndege ya Kampuni hiyo mwezi Desemba 2014 ilianguka katika bahari ya Java na kusababisha vifo vya abiria 162 baada ya mfumo wa rada wa ndege hiyo kutofanya kazi huku ikiwa angani.