Kampuni inayojihusisha na kukodisha ndege binafsi ya huko Las Vegas nchini Marekani iitwayo ‘The Love Cloud’ imeendelea kuzinadi safari zake za kustaajabisha kwa kasi kupitia ndege yake ambayo inayowawezesha wasafiri wapendanao kufanya tendo la ndoa wakiwa angani.
‘The Love Cloud’ wameweka wazi kuwa itamlazimu mteja wao kulipia kiasi cha pesa kisichopungua Usd 1000 ambazo ni sawa shilingi milioni 2,305,500 za Kitanzania kwa dakika 45 pekee ili kuweza kushiriki tendo la ndoa akiwa angani wakitumia ndege ya kampuni hiyo.
Vile vile kampuni hiyo inasema wapenda nao wanaweza kulipia hadi Usd 15000 ambazo ni sawa na Shilingi milion 3,457,000 li kuweza kuitumia ndege hiyo kwa lisaa limoja wakiwa angani.
Hii ni ndege isiyoruka nje ya jiji la Las Vegas, hivyo safari zake huenda mpaka futi 5,380 ikiambaa uwanda wa jiji hilo.
“Tumeweka mfumo huo ili kuzidi ndege nyingine yoyote ulimwenguni. Mambo ya ndani ya kimahaba yaliyotengenezwa maalum ni pamoja na mfumo wa sauti na mwanga, kuna shuka nyekundu za satin, mito na mazingira mazuri ya kufanyia tendo, ikiwa ni pamoja na godoro lililotengenezwa maalum ili kuifanya safari yako ya ndege iwe rahisi sana.”
“Wewe na rubani mnatenganishwa na mlango wa pazia maalum. Rubani pia ana kifaa cha kuzuia kelele ili wewe na mshirika wako muwe na faragha kamili katika safari yote ya ndege.
Kwa hivyo pindi tu unapopanda kumbuka tu kukaa, kupumzika, na kufurahia uzoefu wa kipekee ukiwa angani na mpenzi wako.” Alisema mmoja wa washirika wa kampuni hiyo.