Serikali inatarajia kuanza kutumia Ndege zisizo na rubani (Drones), kukabiliana na uharibifu wa visumbufu vya Mazao Shambani, ambapo pia imewasisitiza Wakulima kufanya Kilimo chenye tija kitakachowasaidia kujiinua kiuchumi.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ameyasema hayo wakati wa hafla ya kupokea Ndege kubwa isiyo na Rubani, yenye uwezo wa kupulizia dawa na Viuatilifu Hekta 20 kwa saa moja, pamoja na Vishkwambi 370 vyenye thamani ya shilingi 364 Milion.

Amesema, “Vifaa hivi ni muhimu katika Sekta ya Kilimo na Drone hii kubwa kuliko nyingine inakwenda kuwa suluhisho la visumbufu vya Mazao Shambani, niwashkuru sana WFP kwa kutupatia vifaa hivi, ambavyo Vishkwambi vinakwenda kugawiwa kwa Maafisa Ugani kwa ajili ya kukusanya taarifa mbalimbali za Kilimo.”

Wizara ya Kilimo pia imekutana pamoja na wadau wa Shirika la Kimataifa la Mpango wa chakula Duniani – WFP, kwa ajili ya kujadili uundaji wa kituo kimoja cha kupokea na kufuatilia taarifa, ikiwemo kudhibiti visumbufu hivyo vya mazao.

Gari la Maiti latumika kusafirisha Bangi, harufu yawakamatisha
Wataalam, Mawaziri wa Afya wapanga kuyakabili magonjwa