Ndege mbili za zamani za kijeshi zimegongana angani na kuanguka wakati wa onyesho la anga la la WWII Dalas, katika jimbo la Texas nchini Marekani, huku ikiwa haijabainika ni watu wangapi walikuwapo katika ndege hizo ingawa taarifa za awali zinaonesha wote wamefariki.
Mgongano huo wa ndege umetokea hapo jana Jumamosi Novemba 12, 2022 na ulisababisha ndege hizo kuporomoka chini na kulipuka na kutoa miali ya moto, na kusababisha moshi mweusi kutanda angani, huku mamlaka za usalama zikisema hakuna majeruhi kwa watu waliokuwa ardhini.
Shirikisho la anga la FAA, limesema onesho hilo lilihusisha mshambuliaji wa enzi ya Vita vya Pili vya Dunia aina ya Boeing B-17 Flying Fortress na mpiganaji wa Bell P-63 Kingcobra akiruka kwenye Wings Over Dallas Airshow kwenye Uwanja wa Ndege wa Dallas Executive, kulingana na Utawala wa Shirikisho la Anga (FAA).
Aidha baada ya ajali hiyo, Maafisa wa uwanja wa ndege wamesema Wafanyakazi wa dharura walikimbia hadi eneo la ajali huku rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Kumbukumbu ya Jeshi la Anga (CAF), Hank Coates akisema kikundi kilichojitolea kuhifadhi ndege za vita vya Vita vya Kidunia vya pili, cha B-17 huwa na wafanyakazi wawanne hadi watano.