Wakazi wa mji mmoja wa Marekani wameonywa kutowatilia maanani ndege ambao wanamuonekano wa kulewa, wanaosumbua maeneo kadhaa ya mji.

Polisi katika mji wa kaskazini mwa Minnesota wa Gilbert wamedai kupokea ripoti juu ya ndege hao ambao wanarukaruka kwenye madirisha, magari na kuonekana wamechanganyikiwa.

Hali ya kulevya ya ndege hao na kufanya fujo inaelezwa kunatokana na ulaji wa matunda yaliyostawi mapema kabla ya msimu wa baridi.

Mkuu wa polisi alieleza kuwa ndege wadogo hawana uwezo wa kuhimili kilevi wanachokipata kutoka katika matunda hayo tofauti na ndege wakubwa.

Aliongeza kueleza kuwa hakuna haja ya kuwachukulia hatua za kisheria kwa sababu ndege hao watarejea kwenye hali yao ya kawaida ndani ya muda mfupi.

Hata hivyo wamewashauri wakazi wa eneo hilo kuwaita polisi kama wakiona fujo za ndege hao zimezidi.

tangazo

Wenyeji wa eneo hilo wameandika maoni yao katika tangazo ambalo linaeleza juu ya ndege wanaolewa

“jamani, hii inaeleza kwa kina kuhusu ndege hao wanaorukaruka katika madirisha hivi karibuni”, mmoja wa wakazi aelezea.

“Maelezo haya yanaeleza wazi ni kwa nini niliwapiga ndege saba waliokuwa wanacheza kwenye gari langu” mkazi mwingine alisema

Video: Mtoto wa Suge aonesha video anayodai ni Tupac ‘yuko hai’ Malaysia
Olympic Lyon yatawala tuzo ya Ballon d'Or kwa wanawake