Ndege ndogo ‘Helkopta’ ya jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania ( JWTZ), imewasili uwanja wa ndege wa Seronera uliopo ndani ya hifadhi ya taifa Serengeti majira ya mchana, kuchukua mwili wa mtoto wa Mkuu wa Majeshi Tanzania, Jenerali Vanance Mabeyo, Nelson Mabeyo ambaye amefariki kwenye ajali ya ndege iliyotokea leo ndani ya hifadhi hiyo.

Nelson alikuwa rubani wa ndege ya kampuni ya Auric air yenye namba 5H – AAM, alipata ajali katika uwanja huo akiwa na rubani mwanafunzi Nelson Orutu ambaye pia alifariki dunia papo hapo.

Awali miili ya wawili hao ilihifadhiwa katika Zahanati ya Soronera na kusubiri taratibu za kusafirishwa.

Kwa upande wa mwili wa rubani mwanafunzi Nerson Urutu, umechukuliwa na ndege ya kampuni ya Auric na kupelekwa mkoani rusha kwa taratibu za mazishi.

Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Massana Mwishawa amesema kuwa tukio hilo limewashtua sana kwakuwa ni mara ya kwanza kutokea na kusababisha vifo vya watu.

Kwaupande wa Kamishna wa Uhifadhi kanda ya Magharibi, Martini Loiboki ameomba taratibu za uchunguzi zifanyike kwa wakati.

 

 

Mtalii afa maji akimchumbia mpenzi wake
Video: Tumaini jipya kwa walinzi baada ya kusajiliwa PSGP