Ndege ya kijeshi al Urusi jana ilianguka katika eneo la pwani ya Syria na kusababisha vifo vya marubani wote wawili.

Waziri wa Ulinzi wa Urusi amesema kuwa ndege hiyo haikulipuka baada ya kuanguka na kwamba chanzo cha ajali hiyo kinaweza kuwa tatizo lililotokea katika injini zake.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la Tass, wizara imeeleza kuwa ndege hiyo aina ya Su-30 ilianguka muda mfupi baada ya kupaa ikitokea katika kambi ya kijeshi ya Urusi iliyoko Hemeimeem nchini Syria.

Urusi inayomuunga mkono rais Bashar Assad imeweka kambi nchini humo na ilianza kuweka ulinzi wa anga tangu mwaka 2015.

Hii sio ajali ya kwanza kwa ndege ya kivita ya Urusi nchini Syria, Machi mwaka huu, ndege nyingine ilianguka wakati ikitua katika eneo la Hemeimeen na kusababisha vifo vya watu 39 waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

Serikali ya Urusi ilielezea ajali hiyo kuwa imetokana na matatizo ya kiufundi na kwamba haikutunguliwa kama ilivyokuwa ikielezwa na baadhi ya vyanzo vya habari.

 

Urusi imekodi eneo la Hemeimeem na kuweka kambi ya jeshi, karibu na pwani ya Mediterranean.

Ommy Dimpoz aweka wazi wanaomuomba awaoe
Video: Dkt. kutoka Muhimbili azungumzia Ugonjwa wa Pumu