Nchini Somalia ndege iliyobeba vifaa vya misaada kwa ajili ya kukabiliana na virusi vya Corona nchini humo imeanguka na kuuwa watu sita.
Waziri wa Usafirishaji, Mohamed Salad ameeleza kuwa ndege hiyo iliyokuwa ikotokea Mogadishu kuelekea Baidoa, kisha ikaendelea na safari mpaka Mjini Bardale ambapo ilianguka.
Aidha Waziri amesema miili mitano imepatikana na tayari ameshatuma timu ya uchunguzi.
Hata hivyo, Salad hajaweka wazi chanzo cha ajali, lakini Waziri wa zamani wa Ulinzi Abdirashid Abdullahi Mohamed ameliambia Shirika la Habari la Reuters kuwa amezungumza na shahidi ambaye amesema inawezekana ndege hiyo imedunguliwa.