Ndege ya India iliyokuwa ikisafiri kutoka Mumbai kwenda London Uingereza imelazimika kuahirisha safari ikiwa angani kwa kuhofia Panya.

Taarifa iliyotolewa na BBC imeeleza kuwa, Ndege hiyo aina ya Al 131 ilikuwa imefika Iran lakini mmoja kati ya abiria alieleza kuwa amemuona panya.

Kutokana na taarifa hiyo, rubani wa ndege alielekezwa kuahirisha safari kuhofia Panya huyo na alifanya hivo.

Shirika la ndege la India Air limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kufanya uchunguzi wa kina kwa kuwa panya huyo hakuonekana baada ya taarifa hizo.

Shirika hilo limeeleza kuwa uamuzi wa kusitisha safari hiyo ulifanywa kwa usalama wa abiria.

 

Farid Mussa Kusaka Maisha Hispania
Ame Msimu: Mafunzo Bingwa Kombe La Mapinduzi