Maafisa wa uwanja wa ndege wa Almaty wamethibitisha kuwa takribani watu 14 wamefariki baada ya ndege iliyokuwa imewabeba abiria 98 na wafanyakazi kuanguka nchini Kazakhstan.

Wamesema kwamba ndege hiyo ya Bek Air aina ya FlightZ92100, ilianguka muda mfupi baada ya kupaa katika uwanja wa Almaty mapema leo na majeruhi 35 wakiwemo watoto wanne wamepelekwa hospitali.

ndege hiyo ilipoteza mawasiliano mwendo wa saa moja na dakika 22, kabla ya kugonga kizuizi kimoja na kuangukia nyumba ya ghorofa mbili.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Reuters, ndege hiyo ilikuwa ikitoka mji mkubwa wa Almaty ikielekea mji mkuu wa Kazakhstan, lakini kulikuwa na hali mbaya ya hewa huku kukiwa na ukungu mzito katika eneo la mkasa ijapokuwa bado haijulikani ni nini kilichosababisha ajali hiyo.

Rais wa Kazakhstant, Qasym-Jomart Toqayev ameeleza kusikitishwa na ajali hiyo na kuwaomboleza waathiriwa huku akiahidi kwamba wale wote waliohusika wataadhibiwa kulingana na sheria.

Bek Air ilianzishwa 1999, ikilenga kuwabeba watu maarufu lakini Siku hizi kampuni hiyo inajielezea kuwa kampuni ya bei ya chini zaidi nchini Kazakhstan. Ina ndege 100 aina ya Seven Fokker.

Hiki hapa kilicho waangamiza Azam FC
Ripoti: Mtandao wa kuuza watoto hatari kama ‘wa unga’, wana mbinu na nguvu