Ndege ndogo aina ya Cessna 172, jana  iligonga jengo lililoko katika Manispaa ya Anchorage, Alaska nchini Marekani na kusababisha kifo cha mtu mmoja.

Kwa mujibu wa ripoti ya FBI kuhusu tukio hilo, rubani aliyekuwa anaiendesha ndege hiyo aliyefahamika kwa jina la Doug Demarest mwenye umri wa miaka 42 alifariki. FBI ambayo inachunguza tukio hilo imeeleza kuwa rubani huyo aliirusha ndege hiyo bila kibali.

Ngege aina ya cessna-172

Ngege aina ya cessna-172

Ndege hiyo inamilikiwa na shirika la kiraia linalosaidia kufanya ukaguzi wa usalama angani, utafutaji na uokoaji katika majanga mbalimbali.

 

Wekundu Wa Msimbazi Simba Waigomea Etoile Du Sahel
Ripoti: Viongozi 10 waandamizi wa ISIS wauawa Syria, Iraq