Ndege ya abiria yenye watu 190 imeanguka katika uwanja wa ndege, kusini mwa Kerala nchini India na kusababisha vifo vya watu 18, kwa mujibu wa Serikali ya nchi hiyo.

Ndege hiyo aina ya Boeing 737 iliyokuwa inasafiri kutoka Dubai, ilikumbwa na mvua yenye upepo mkali iliyosababisha kuanguka na kugawanyika vipande viwili.

Waziri Mkuu, Narendra Modi ametuma salamu za rambirambi akieleza kuwa ameumizwa na taarifa ya kuanguka kwa ndege hiyo.

Kwa mujibu wa Waziri anayeshughulikia eneo la Kerala, Pinarayi Vijayan, majeruhi walikimbizwa katika hospitali mbili za Calicut na Malappuram. Ameeleza kuwa kati ya makumi waliojeruhiwa, 156 kati yao wako katika hali mbaya. Watoto wadogo 10 walikuwa miongoni mwa abiria hao.

Ndege hiyo ilianguka Jana majira ya saa moja na dakika 40 jioni kwa saa za India, ikijaribu kutua kwa mara ya pili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Calicut. Jaribio la kwanza la kutua lilishindikana kutokana na mvua kali iliyoambatana na upepo mkali.

Waziri wa Anga, Hardeep Singh Puri aliandika katika mtandao wa Twitter kuwa ndege hiyo ilianguka kutoka umbali wa futi 35 na kukatika vipande viwili. Aliongeza kuwa Mamlaka za nchi hiyo zimeanza kufanya uchunguzi wa kina kuhusu ajali hiyo.

SADC ngazi ya makatibu wakuu wajadili kuboresha rasimu za nyaraka za kisera

Lissu kuchukua fomu ya urais leo

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Agosti 9, 2020
SADC ngazi ya makatibu wakuu wajadili kuboresha rasimu za nyaraka za kisera

Comments

comments