Klabu ya  Azam FC hii leo imepata neema ya mkataba mpya wa NMB baada ya kuonekana kuutendea haki mkataba wao wa awali wa benki hiyo hivyo imewaongezea mwingine wa mwaka mmoja ambao utawasaidia kupambana kuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Akizungumza wakati wa kusainishana mkataba huo Mkurungezi wa NMB,Imeko Bussemaker, alisema kwamba wameamu kuingia mkataba mpya na Azam baada ya kuridhishwa na ule wa awali, hivyo kwakuwa wao wamekuwa wakishiriki kikamilifu katika masuala ya michezo, wanaamini Azam itaongeza wigo mkubwa katika kuzalisha wachezaji wachanga hapa nchini ambao wataiinua hata timu ya taifa wanayoidhamini pia.

Naye Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdul Mohamed, yeye amewashukuru NMB kwa udhamini huo “Niwashukuru sana kwa hili lakini huku napenda niwaahidi kua siku chache zijazo nitarudi hapa tena kuwakabidhi Kombe la Ligi Kuu Bara, kwani tunaamini hadi  mwisho wa msimu mambo yatanyooka maana farsafa yetu kwa sasa tunaendelea kupambana kimyakimya kama tunamfukuza mwizi,” alisema Abdul.

Mkhitaryan kutumia jezi ya Man Utd kutoa msaada
TFF yakataa viwanja vitatu kombe la shirikisho