Mwanadada anaekamata namba moja kwa ubora duniani Garbine Muguruza amejiondoa katika michuano ya Tennis ya China Open.

Muguruza mwenye miaka 23 alipoteza seti ya kwanza kwa 5-1 mbele ya Barbora Strycova wa Jamhuri ya Czech.

Mwanadada huyo ambaye ni bingwa wa michuano ya Wimbledon aliumia kiwiko cha mkono na kumfanya ashindwe kuendelea namchezo huo.

Baada ya timu ya madaktari kuwasili, ilisemekana hatoweza kumalizia ngwe iliyokuwa imesalia.

Muguruza amesema hakupenda kabisa kuishia katikati ya michuano hiyo.

Simba SC waomba radhi mkanganyiko wa rangi za jezi
Donald Ngoma aiweka roho juu Young Africans