Naibu Spika wa Bunge la Tanzania na mbunge wa jimbo la Kongwa, Job Ndugai amekanusha tuhuma za kumshambulia kwa fimbo Dkt. Joseph Chilongani hadi kupoteza fahamu, akimuadhibu kwa kumpiga picha wakati anafanya fujo katika mkutano wa kampeni za kura za maoni.

Ndungai alisema kuwa yeye hakumpiga Dkt Joseph Chilongani katika lake kama ilivyodaiwa, bali alipiga simu iliyokuwa inamrekodi.

“Nilishamuonya mara kadhaa aache kujifanya mwandishi wa habari kwa kuchukua video tena akinilenga mimi tu, lakini hakusikia. Nilichofanya niliigonga ile simu aliyokuwa akiitumia kuchukua video,” Alisema Ndugai.

Akizungumzia tuhuma za Ndungai, Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime alisema kuwa jeshi la polisi limekamilisha upelelezi juu ya tukio hilo na kwamba hivi sasa wanasubiri ripoti ya daktari kuhusu afya ya mgonjwa.

“Tunataka kupata ripoti ya daktrai aliyemhudumia Dkt. Chilongani kabla hatujachukua hatua zaidi za kisheria,” alisema na kuongeza kuwa jeshi hilo lilimshikilia Ndungai na kumuachia baadae kwa dhamana.

Kwa upande wake Dkt. Chilongani, alisema kuwa hali yake bado haijaimarika kutokana na shambulio hilo na kwamba tetesi za kupoteza maisha zilimshtua.

“Hali yangu sio nzuri kwa sababu nina tatizo la presha na hii imeongezeka kutokana na mshtuko nilioupata baada ya kusikia tetesi kuwa nimefariki. Watu wengi walikuja hospitalini kunitembelea na wengine walianza kuuliza kama niko hai au kweli nimepoteza maisha,” alisema Dkt. Chilongani.

Aliongeza kuwa kwa kuwa hali yake bado ni mbaya, ameshindwa kushiriki katika mchakato wa kampeni za kura za maoni kwa kuwa naye ni mgombea anaewania nafasi ya kwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM.

 

Depay Atisha Mapokezi Ya Man Utd
Zokora Kumalizia Soka Lake Ligi Kuu Ya India