Spika Job Ndugai amezungumza amesema pamoja na kuwepo kwa kanuni za Bunge zipo pia kanuni za uendeshaji wa shughuli za Bunge kwa wabunge wa CCM kama chama tawala na kwa wabunge wa kambi pinzani ambazo zote ni sehemu ya uendeshaji wa shughuli za Bunge.
Amesema kuwa hoja haiwezi kujadiliwa bungeni kama muwasilishaji wa hoja hiyo hajaiwasilisha kwenye chama chake ili ijadiliwe huko na kupitishwa na kujadiliwa bungeni.
-
Majambazi wavunja kanisa la Mt. Theresia, Mbezi
-
Video: Mbowe atoa msimamo mkali, Vyama vinavyovunja sheria sasa kufutwa
Ndugai ametoa kauli hizo pindi alipokuwa akijibu hoja ya Hussein Bashe ambaye ni mbunge wa Nzega mara baada ya kuandika barua yenye hoja binafsi kwa Katibu wa Bunge bila kufuata kanuni na taratibu za uendeshaji wa shughuli za Bungeni.
Ndugai amesema Bunge bado halijapokea hoja hiyo mpaka itakapojadiliwa na chama chake na kuipitisha ndipo itakapowasilishwa na kujadiliwa na wabunge kutoka pande zote mbili.
Ikiwa vikao vya kamati ya Bunge vinaendelea, Bashe amemuandikia barua Katibu wa Bunge na kuwasilisha hoja yake binafsi akitaka kuundwa kwa tume teule ya kuchunguza matukio ya uhalifu yanayotokea nchini.