Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ametoa ufafanuzi kuhusu suala zima la Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali akisema kuwa kitendo alichokifanya ni kulidharirisha bunge hivyo anapaswa kuripoti kwenye kamati ya maadili ya bunge.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa mkaguzi huyo alipaswa kuwa balozi wa kuitangaza nchi ili iweze kupata misaada na wawekezaji.

Akizungumzia suala la Zitto Kabwe kufungua kesi ya kutetea ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, amesema kuwa amekuwa akipata wakati mgumu kuwa na kiongozi muongo kama huyo ambaye amekuwa akitunga vitu ambavyo si vya kweli.

”Unajua huyu Zitto ananipa wakati mgumu sana, ni kiongozi mmoja muongo sana anadanganya danganya watu na kujificha kwenye vikorido vya hapa Dar es salaam wakati wabunge wenzie wako Dodoma, namuangalia tu lakini itafikia kipindi ntamchukulia maamuzi magumu,”amesema Ndugai

Hata hivyo, Ndugai ameongeza kuwa kamati ya maadili ya bunge inaendelea kumsubili Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Assad ili kuweza kujibu tuhuma zinazomkabili za kulidharirisha bunge akiwa nje ya nchi.

Polisi Njombe waeleza matukio ya utekaji na mauaji
Wanafunzi 14 wajeruhiwa na radi mkoani Kagera