Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amesema Jimbo la Hai limepata Mbunge hivi sasa, akiongeza aliyekuwepo kabla ya hapo alikuwa anazurura kila mahali

Ndugai ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma akisema, “Alikuwa haulizi maswali Bungeni, haeleweki lakini sasa Mbunge mnaye kabisa”

Kauli yake imekuja baada ya Mbunge Saasisha Mafuwe kuhoji ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya kumaliza mgogoro wa Ardhi uliopo kati ya Wananchi na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (KIA).

Mbunge huyo amesema mgogoro huo umekuwepo muda mrefu na kusababiaha wananchi kukosa maeneo ya malisho na kuishi kwa wasiwasi kwenye maeneo yao.

Takukuru yamalizana na Kakoko wa TPA, bado ‘chujio’ la CAG
Rais Samia atuma ujumbe wa Ramadhani