Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limemchagua mbunge wa Kongwa, Job Ndugai, kuwa Spika wa Bunge la 12, baada ya kupata ushindi wa kura kwa asilimia 99.7.

Katika uchaguzi uliofanyika hii leo Novemba 10, 2020, Bungeni Dodoma, Ndugai amepigiwa kura na wabunge wateule 344 kati ya wabunge 345 na kura ya hapana ilikuwa ni moja.

Baada ya ushindi huo Ndugai aliapa kiapo cha uaminifu na kisha kuanza kazi ya kuongoza shughuli za bunge.

Spika Ndugai amesema kuwa haitakuwa kazi rahisi kwake kwa Bunge la 12 kwa kutimiza majukumu ya kupitisha bajeti na sheria mbalimbali.

Awali akiomba kura kwa wabunge hao, Ndugai amesema kuwa Bunge la 12 litakuwa ni Bunge bora na mfano wa kuigwa na kwamba katika Bunge hilo hakutakuwa na kambi rasmi ya upinzani Bungeni kwa kuwa hawajatimiza asilimia 12.5, kwa mujibu wa kanuni za Bunge.

TMA: Mvua kuwa chini ya wastani Manyara
Ansu Fati hadi Machi 2021