Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema kuwa Watanzania na wafanyakazi sasa wanapaswa kutumia ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) pindi wanapofanya safari sehemu ambazo kuna vituo vya shirika hilo.

Ndugai amesema hayo leo Desemba 23, 2018 katika mapokezi ya ndege mpya ya Airbus A220-300 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.

Amesema Tanzania ilikuwa inachekwa hadi na nchi ndogo kutokana na kukosa kitu cha kujivunia na hivi sasa kipo kitu cha kujivunia na Watanzania wanapaswa kuunga mkono juhudi hizo na kuwa wazalendo.

“Tuunge mkono juhudi ili kuwezesha ‘graph’ ya mauzo na mapato ya ndege zetu kuendelea kupanda kila siku na nyie bodi ya ATCL endeleeni kusimamia suala hili ili isiwe kama ile iliyopita,” amesema.

Amesema kuwa awali Bodi iliyopita ilikuwa ikiangalia tu mambo, mapato yanashuka ipo tu, yanaendelea kushuka ipo tu hadi yanafika sifuri haijafanya chochote.

Hivyo ameitaka Bodi mpya kuhakikisha hilo halotokei tena badala yake ichape kazi ili kuliendeleza shirika hilo.

“Bodi iliyopita ilikuwa ikiangalia tu mambo, mapato yanashuka ipo tu, yanaendelea kushuka ipo tu hadi yanafika sifuri haijafanya chochote, jamani tuhakikishe hilo halitokei tena,” amesema Ndugai.

Ndege hiyo itakakuwa inafanya kazi zake ndani na nje ya nchi na inauwezo wa kubeba abiria 132 huku 12 kati yao wakiwa ni wa daraja la biashara.


Video: Rais Magufuli akipokea ndege mpya ya Tanzania

Rais Magufuli awatangazia hatari watendaji 100 wa Serikali, wapo mawaziri na wabunge
Live: Rais Magufuli akipokea ndege mpya ya Tanzania

Comments

comments