Kijana Jon Luc McLoughlin, mwenye umri wa miaka 26, mkazi wa Poole Dorset nchini Uingereza, amehukumiwa kwenda jela wiki 16, baada ya kumpiga ngumi Mbwa wake hadi kufa.

Hukumu hiyo ilisomwa juzi Novemba 28, 2019 na kuhudhuriwa na wanaharakati 25 wa Wanyama, pamoja na Mama yake mzazi na wadogo zake wawili.

Baada ya kuhukumiwa mdogo wake, Alec Mackay, alimedai kuwa hukumu ya wiki 16 ni ndogo na angetakiwa afungwe angalau mwaka 1.

“Ingekuwa Binadamu angefungwa kifungo cha muda mrefu sana, kwakuwa sisi wote ni viumbe hai angeongezewa kifungo kidogo.”ameeleza Alec.

IGP Sirro alivyokimbiwa na mchumba kisa Mzawa wa Mara

Matthew Knight, Mwendesha Mashtaka wa Haki za Wanyama nchini humo kutoka (RSPCA), amesema kuwa Jon alimpiga ngumi Mbwa wake hadi kufa na kumtupa karibu na mtaani kwao.

Mahakama ya Poole imepata taarifa kuwa Jon-Luc McLoughlin, alikaa na Mbwa huyo kwa Mwezi 1 pekee na hatimaye kumuua huku chanzo kikitajwa kuwa ni matatizo binafsi.

Muhimbili yafanya upasuaji wa kurekebisha jinsi tata
Video:Mwakinyo ameshinda kwa haki? Promota, mashabiki, wafilipino wafunguka