Familia ya Kardashians inaendeleza wimbi la vimbwanga na matukio yanayowacha watu midomo wazi, matukio ambayo tunaweza kuyatafsiri kama ‘ukichaa wa umaarufu’.

Mdogo wa Kim Kardashian, Kendall Jenner, amefuata nyayo za ndugu zake baada ya kukubali ofa ya kupiga picha akiwa kifua wazi ikiwa ni sehemu ya tukio la kusapoti kampeni ya Calvin Klein iliyopewa jina la ‘The Original Sexy’.
Binti huyo mwenye umri wa miaka 19 amepozi katika picha mbalimbali akionesha sehemu za makali na kifuani huku mikono yake ikisaidia kuzificha baadhi ya sehemu hizo.
KEN

Familia hiyo inayoundwa na mastaa wa ‘Keeping Up With the Kardashians’ inaendeleza wimbi la vituko ikiwa ni miezi michache imepita baada ya baba yao wa kambo, Bruce Jenner kubadili jinsi yake na kuwa na muonekano wa kike. Bruce hivi sasa anajiita Caitlyn Jenner.

Ibra Kadabra Adhamiria Kukutana Na Hasimu Wake Ujerumani
Avril Ahamishia Taarifa Za Ujauzito Wake Kwa Ndugu Yake