Katika hali isiyotarajiwa, ndugu wa mgonjwa aliyepata ajali ya pikipiki wamempiga Daktari wa Hospitali ya Rufaa ya Ligula Mkoani Mtwara, aliyekuwa anamhudumia mgojwa wao.

Daktari huyo aliyekumbwa na mkasa huo ambaye hakutaka jina lake litajwe na vyombo vya habari alieleza kuwa alipokea kipigo kutoka kwa ndugu wa mgonjwa huyo baada ya kumuandia rufaa kwenda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbini (MNH).

Alisema kuwa alichukua uamuzi huo baada ya vipimo kuonesha kuwa mgonjwa alikuwa amevunjika mfupa wa mguuni mara kadhaa na kwamba hospitali hiyo haina uwezo wa kumpa matibabu husika kulingana na madhara aliyoyapata katika ajali iliyotokea Jumamosi iliyopita, lakini alishangazwa na uamuzi wa ndugu hao kuonesha kupinga uamuzi huo kabla ya kuanza kumpiga.

Kutokana na hali hiyo, madaktari wa hospitali hiyo walianza mgomo na kukaa makundi madogomadodog wakiacha kutoa huduma kwa madai kuwa wanahofia maisha yao. Madaktari hao walilaani kitendo alichofanyiwa mwenzao.

Baadhi ya wagonjwa walilamika kutopata matibabu tangu walipowasili hospitalini hapo majira ya mchana hadi jioni huku wakiwasihi madaktari kuwaokoa wagonjwa ambao wanaweza kupoteza maisha yao kutakana na mgomo huo.

Hata hivyo, mwandishi wa gazeti la The Citizen alipata nafasi ya kuzungumza Mkuu wa Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara, Dk. Shaibu Maarifa ambaye alieleza kuwa hakuwa na taarifa za kuwepo kwa mgomo hospitalini hapo kwa kuwa alikuwa nje ya ofisi.

Hivi karibuni, madaktari nchini walianza kulalama wakidai kunyanyaswa na wagonjwa katika hospitali za umma. Madaktari wa Hospitali ya Wilaya ya Butimba (Nyamagana) mkoani Mwanza pia waligoma hivi karibuni kwa saa kadhaa wakidai kunyanyaswa na wagonjwa, hali iliyopelekea aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mlongo kuingilia kati.

 

 

Hassan Isihaka Atoka Jela Ya Msimbazi
'Nyoka' watumika Wizi wa Maji Dar