Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile amelipa siku 90 Shirika la Posta Tanzania (TPC) kuboresha utendaji kazi na ufanisi katika kuhudumia wateja na wananchi kwa ujumla katika shughuli za kila siku za uendeshaji wa shirika hilo.

Dkt. Ndugulile ameyasema hayo kwa Bodi, Menejimenti na wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania wakati wa ziara yake ya kutembelea Shirika hilo, Dar es Salaam kwa lengo la kufahamu utendaji kazi wa Shirika ili kuhakikisha kuwa linahudumia vema wananchi.

Aidha Ndugulile ameitaka TPC ipitie mikataba yake ambayo haina maslahi kwa Shirika na isimamie vizuri rasilimali zake ikiwemo viwanja, ofisi na magari kwa kuwa rasilimali ni mtaji na mtaji sio fedha ili rasilimali hizo zitumike kuongeza mapato ya Shirika.

Sambamba na hilo, ameiagiza  Wizara yake kushirikiana na TPC kufanya mapitio ya sera na sheria ya posta ili ziweze kuendana na mabadiliko ya teknolojia duniani ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Naye Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Kundo Mathew ameipongeza TPC kwa kutengeneza mfumo wa taarifa wa Posta ambao unasimamia na kufuatilia uendeshaji wa Shirika, malipo na ukusanyaji wa mapato, na taarifa za watumishi

Arteta: Sijabadili mipango ya usajili
Isco kuhamia England, Wijnaldum kutimkia La Liga