Safari moja huanzisha nyingine, msemo huu uko chanya na hai kwa Diamond Platinumz ambaye kila siku anaonekana kupiga hatua kubwa katika muziki wake.

Tumezoea kuwa wasanii wa Afrika ndio huwa na kiu ya kuwafuata wasanii wakubwa wa Marekani kuwaomba collabo, lakini nyota ya Diamond imeng’aa kama ile ya mashariki na kumgusa mwandishi na mwimbaji mkubwa wa RnB Marekani, Ne-Yo ambaye alimtafuta na kuzungumzunga nae ili wafanye kitu.

Diamond ambaye yuko Durban, Afrika Kusini akisubiri tuzo zake tatu za MTV/MAMA zitakazotolewa leo jijini humo, ameandika kwenye instagram kilichotokea.
“Wakati nazungumza na D’Banj @salaam_sk alinifata na kunambia Ne-Yo anakutafuta anataka kukuona… ungependa kujua kilichofuata??? Kaa tayari na TV, Radio yaani kiufupi Media zako soon utayasikia… #MTVmama2015”

Hata hivyo, msanii wa Tip Top Connection, Madee alikoreza maandishi kwa kuweka wazi kuwa kinachotakiwa kufanyika ni collabo.

“Tsup boss … I knw deal done chibu vs neyo @babutatl,” aliandika Madee katika post yake inayomuonesha Babu Tale akiwa na Ne-Yo. Baada ya muda Babu Tale alijibu kwa post hiyo, “Done”.

My Take: Bidii kubwa na uwekezaji mkubwa katika muziki wake na timu nzuri ya menejimenti ya Diamond Platinumz inaweza kuwa sababu kubwa ya jina la Diamond anaewania vipengele vitatu kwenye tuzo za MTV/MAMA2015, kumshtua Ne-Yo aamini kama angetaka kukutana na wasanii wakubwa wa Afrika angekuwa hajafanikisha bila kumuona Chibu Dangote kutoka Tandale, Dar es Salaam, Tanzania.

Inaeleweka wazi kuwa Diamond ndiye msanii anaye-trend zaidi kwenye mitandao ya kijamii, ukubwa wa nyimbo zake na jinsi zinavyopata nafasi kubwa na kuongoza kwenye chart za media kubwa Afrika, plus kutajwa mara nyingi kwenye tuzo zote kubwa. Diamond yuko kimkakati na hafumbi jicho lake bila kuwaza kesho atapiga hatua gani kwenda mbele. Hivyo, kutafutwa na NE-Yo sio ‘kuokota dodo kwenye muembe’, ni matokeo ya kawaida ya bidii yake kubwa.

Kwa bidii kama hizi za Daimond na wasanii wengine wanafanya kila njia nzuri kuhakikisha wanapenya kwenye anga za kimataifa, ni sababu iliyomfanya rais Kikwete kuwakumbuka wasanii kwenye hotuba yake ya kufunga bunge la kumi akisema wasanii wa hawa wanatuwakilisha vizuri kimataifa na wanapaswa kupewa sapoti kubwa.

Picha: Kim Kardashian Azitosa Make Up Kwenye Jarida La Vogue
Tanzia: Banza Stone Atangulia Mbele Ya Haki