Mkali wa ‘Miss Independent’ na ngoma nyingi kubwa, Ne-Yo anatarajiwa kuubariki msimu wa tatu wa ‘Coke-Studio Africa’ mwaka huu nchini Kenya.

Neyo ambaye mwezi uliopita alitua nchini Afrika Kusini na kutumbuiza kwenye Tuzo za MTV/MAMA 2015, ataungana na mastaa wengine wa Afrika kutengeneza muziki mzuri na kutumbuiza katika show hiyo.

Coke Studio hurekodiwa kabla na kurushwa kwenye vituo vikubwa vya runinga Afrika. Huwaleta pamoja wasanii wengi wakubwa kufanya kazi pamoja kuongeza chachu ya vipaji Afrika. Pia, huwapa nafasi wasanii wachanga kufanya kazi na wasanii wakubwa.

Show hii huzaa collabo kadhaa baada ya wasanii kujenga urafiki wanapokuwa jijini Nairobi wakifanya mazoezi na kurekodi. Mwaka jana, Joh Makini alifanya collabo na Chidimna wa Nigeria baada ya kukutana katika show hiyo.

 

Mwanafunzi Wa ‘PhD’ Aliyeua Watu 12 Asamehewa Hukumu Ya Kifo
Zitto Adai Magufuli Sio Msafi, Amhusisha Na Ufisadi Wa Bilioni 87