Mwimbaji wa ‘So Sick’, mwandishi mahiri wa mashairi mwenye vipaji vingi, Chimere Smith maarufu kama Ne-Yo atatua nchini kwa ajili kuwapa burudani watanzania.
Ne-Yo anatarajia kutumbuiza jijini Mwanza, Mei 21 kwenye Tamasha kubwa la kila mwaka linalowakutanisha wasanii wengi ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Jembeka, linaloandaliwa na kituo cha radio cha Jembe Fm.
Neyo anaikanya ardhi ya Tanzania kwa mara ya kwanza na mara ya tatu Afrika Mashariki.