Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetupilia mbali malalamiko yaliyowasilishwa na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuhusu kauli za mjumbe wa kamati ya kampeni ya CCM, Abdallah Bulemboo alizodai ni za uchechezi.

Kauli ya Bulembo iliyolalamikiwa na Mbowe ni ile aliyokaririwa akieleza kuwa CCM haitaruhusu wapinzani kuingia Ikulu.

Akiongea jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva alisema kuwa kauli alizozitoa Bulembo ni kauli za kisiasa zisizo na mlengo wa kichochezi endapo zitachukuliwa kwa mtazamo chanya.

Alisema kuwa kauli kama hizo hutumiwa pia na upande wa Chadema ambao hueleza kuwa hawataruhusu CCM iendelee na awamu ya tano ya serikali. Kauli ambazo alidai zinatumiwa kisiasa kwa lengo la kuwahamasisha wanaowaunga mkono kupiga kura kwa wingi kuhakikisha wanashinda uchaguzi mkuu na kutowarusu upande wa pili kushinda.

“Bulembo hakusema kuwa watapinga matokeo kama Mbowe anavyodai, kwa sababu hizo ndizo kauli za kichochezi. Mwenye mamlaka ya kutangaza matokeo ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi pekee,” alisema.

Kadhalika, Jaji Lubuva alivitaka vyama vya siasa kuendelea kuzingatia sheria na taratibu husika na kutotumia lugha za matusi na uchochezi katika kampeni zao.

 

Ukawa Wadai Utafiti Twaweza Ni ‘Kichekesho’ Wataja Tafiti Zinazompa Ushindi Lowassa
Tanzia: Waziri Celina Kombani Afariki