Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeifuta adhabu iliyokuwa inamkabili Mgombea Ubunge wa Jimbo la Vunjo, James Francis Mbatia ambaye alizuiwa kufanya Kampeni kwa siku 7 mpaka Oktoba 23.

Mbatia alipewa adhabu hiyo baada ya kukutwa na kosa la kutumia kipeperushi cha Kampeni ambacho hakijaidhinishwa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Vunjo.

Hata hivyo, mara baada ya kutangazwa kwa adhabu hiyo iliyoanza Oktoba 17, mgombea huyo alitangaza kuwa asingetii adhabu hiyo na kuwa ataendelea na kampeni zake.

“Uamuzi huo ni ubatili, kikao kilichofanyika ni batili na tunaendelea na kampeni kama kawaida.” alisema Mkuu wa idara ya Uenezi na Mahusiano wa NCCR-Mageuzi, Edward Simbeye.

Sababu JPM kutopandisha mishahara miaka mitano iliyopita
Pacha waliotenganishwa warejea nyumbani