Tume ya taifa ya uchaguzi NEC imekamilisha kuchambua na kuamua rufaa za wagombea wa ubunge na udiwani baada ya kupitia kumbukumbu zote za rufaazilizowasilishwa.

NEC ilipokea jumla ya rufaa 616 ambapo kati ya hizo rufaa 160 zilikuwa za wagombea wa ubunge, 456 za wagombea udiwani,malalamiko 25 na rufaa zilizojirudia 44.

Katika rufaa 160 za ubunge zilizoamuliwa na tume, wagombea waliorejeshwa ni 66, ambao hawakurejeshwa ni 32, rufaa zilizokataliwa na kuomba kuengua wagombea ni 57 huku rufaa zilizojirudia zikiwa ni tano.

Kufuatia kumalizika kwa kipindi cha pingamizi na rufaa, wagombea waliopita bila kupinwa kwa mujibu wa kifungu cha 44 cha sheria ya taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 ni 20.

Kikongwe wa miaka 99 apokea fidia ya mamilioni
Kigoma kuwa kituo cha biashara ya madini

Comments

comments