Kwa mujibu wa kifungu cha 62 (a) sheria ya Uchaguzi wa Seriakli za mtaaa, Tume ya uchaguzi imeruhusu wapigakura walipoteza vitambulisho vya kupigia kura kupata fursa ya kushiriki zoezi hilo kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani wa kata 43.

Ambapo imesema katika Uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika rasmi Novemba 26 wapiga kura wameruhusiwa kupiga kura kwa kutumia leseni zao za udereva, pasi ya kusafiria pamoja na vitambulisho vya uraia vianvyotolewa na Mamlaka ya Vitambulsho vya Taifa NIDA.

Fursa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, Ramadhani Kailima alipokuwa akitoa mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi wa uchaguzi huo.

Amesema ‘‘Tume kwa kuzingatia kifungu hicho kuanzia uchaguzi huu imetoa maelekezo kwenye mafunzo haya kwamba imekubali vitambulisho vifuatavyo vitumike, moja ni pasi ya kusafiria, pili ni kitambulisho cha taifa kilichotolewa na NIDA na mwisho ni leseni ya udereva’’.

Aidha amefafanua kuwa ruhusa hiyo imetolewa kwa sharti la kwamba majina na herufi yaliyopo kwenye kitambulisho hicho yafanane na majina na herufi zilizopo kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura.

Hata hivyo Mafunzo hayo bado yanaendelea kufanyika jijini Dodoma kuwaandaa wasimamizi wa uchaguzi huo.

Harry Kane, Ronaldo nani kuibeba timu yake leo?
Serikali kuwapunguzia muda wa masomo madaktari