Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa, akiitarifu kuhusu uwepo wa nafasi wazi za Madiwani katika Kata 14 za Tanzania Bara.
Kwa mujibu wa taarifa ilitolewa hii leo Juni 14, 2023 imeeleza kuwa Waziri ametoa taarifa hiyo kwa kuzingatia matakwa ya Kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292.
Kutokana na taarifa hiyo, Tume kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 13(3) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, inatoa taarifa kwa Umma kuhusu uwepo wa uchaguzi mdogo wa madiwani
katika kata 14 za Tanzania Bara.
Kata zinazohusika na uchaguzi huo mdogo ni kutoka halmashauri 13 zilizopo katika mikoa tisa ya Tabora, Tanga, Simiyu, Kilimanjaro, Mtwara, Njombe, Morogoro na Katavi.