Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetangaza uchaguzi mdogo kwa kata tatu za Nyahanga, Igumbilo na Kibosho Kati, ambao haukufanyika Oktoba 28, 2020, kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo karatasi za kura kukosewa pamoja na vifo kwa madiwani wa kata mbili za Nyahanga na Igumbilo.

Taarifa hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa NEC Gerald Mwanilwa, ambaye amesema kuwa Tume imepanga Novemba 16 mwaka huu kuwa ni tarehe ya uteuzi wa wagombea kwa vyama ambavyo wagombea wake walifariki.

Aidha, taarifa hiyo imeongeza kuwa kampeni za uchaguzi kwenye kata hizo, zitafanyika kwa siku 21 kuanzia Novemba 17 hadi Disemba 8, 2020, na uchaguzi huo utafanyika Disemba 8.

Katika hatua nyingine, Tume imesema kuwa kwa kata ya Kibosho Kati, kampeni hazitafanyika kwa kuwa awali walikwishafanya na kuwaomba wapiga kura wajitokeze kwa wingi ili kumchagua diwani wanayemtaka.

Waziri wa elimu Kenya afutiwa mamlaka ya kusimamia watumishi
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Novemba 14, 2020

Comments

comments