Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imewateua madiwani watatu wanawake wa viti maalum, kuziba nafasi zilizokuwa wazi kutokana na vifo vya madiwani wa halmashauri hizo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera walioteuliwa ni Magreth Kaduma ambaye anakuwa Diwani wa Viti Maalum katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe, akiziba nafasi iliyoachwa wazi kutokana na kifo cha aliyekuwa diwani wa halmashauri hiyo, Mwamini Wikesi.

Dkt. Mpango kuzindua miradi hii Mtwara
Rais Mwinyi ateta na wasanii wa Bongo fleva Ikulu