Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) leo Agosti 21, 2017 imeteuwa Madiwani wanawake wa viti maalum ili kujaza nafasi wazi za Madiwani katika Halmashauri mbalimbali Tanzania Bara.
Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa NEC, Kailima Ramadhani imeeleza kuwa Madiwani hao wameteuliwa kwa mujibu wa kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292,.
Amesema kuwa NEC imefanya kikao chake cha kawaida leo Agosti 21, 2017 na baada ya kushauriana na Vyama vya Siasa imewateua Madiwani Wanawake wa Viti Maalum kumi na wawili (12)
Madiwani hao walioteuliwa ni kama ifuatavyo:
NA. | JINA | CHAMA | HALMASHAURI |
|
Ndugu Saida Idrisa Kiliula | CUF | Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa |
Ndugu Sophia Charokiwa Msangi | CCM | Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga | |
Ndugu Shahara Selemani Nduvaruva | CCM | Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali | |
Ndugu Neema K. Nyangalilo | CCM | Halmashauri ya Manispaa ya Ilala | |
Ndugu Farida Zaharani Mohamed | CCM | Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero | |
Ndugu Lucia Silanda Kadimu | CCM | Halmashauri ya Wilaya ya Tabora (Uyui) | |
Ndugu Amina Ramshi Mbaira | CCM | Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu | |
Ndugu Janeth John Kaaya | CHADEMA | Halmashauri ya Wilaya ya Meru | |
Ndugu Sara Abdallah Katanga | CHADEMA | Halmashauri ya Manispaa ya Ilala | |
Ndugu Ikunda Massawe | CHADEMA | Halmashauri ya Wilaya ya Hai | |
Ndugu Tumaini Wilson Masaki | CHADEMA | Halmashauri ya Wilaya ya Siha | |
Ndugu Elizaberth Andrea Bayyo | CHADEMA | Halmashauri ya Mji wa Mbulu |
Aidha, ameeleza kuwa uteuzi huo umefanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa ambaye kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 alitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi uwepo wa nafasi hizo wazi.