Matokeo ya kidato cha sita mwaka 2023 yanaonesha ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 0.26 ikilinganishwa na mwaka jana (2022), huku jumla ya Watahiniwa 104,549 sawa na asilimia 99.23 ya Watahiniwa wote waliofanya mtihani huo, wakifaulu.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania – NECTA, Dkt. Said Mohamed ameyasema hayo wakati kitangaza matokeo hayo hii leo Julai 13, 2023 mjini Zanzibar na kuongeza kuwa watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani huo walikuwa 106, 883 ambapo wasichana ni 47, 340 na wavulana 59, 543.
Amesema, Watahiniwa waliofaulu ni 93,136 ambao ni sawa na asilimia 98.97, hivyo ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 0.26 ikilinganishwa na mwaka jana 2022.
“Wanawake waliofaulu ni 46,707 sawa na asilimia 99.51 wakati Wanaume waliofaulu ni 57,842 sawa na asilimia 99.00 hivyo ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 0.26 ikilinganishwa na mwaka 2022.” amesema Dkt. Mohamed.