Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wajasiriamali kujiamini katika kufanya biashara zao kwa kutumia vitambulisho vya wajasiriamali.
Magufuli ameyasema hayo leo Oktoba 9, wakati wa uzinduzi wa awamu ya tano ya kampeni za CCM zilizofanyika uwanja wa Benjamini Mkapa na ambapo ameeleza kuwa vitambulisho hivyo vitawasaidia kupata mikopo benki na hata kuvitumia kukata bima za afya.
Aidha ameinisha mipango ya miaka tano ikiwemo kuimarisha hali ya usalama, miundombinu, kuboresha afya, kusimamia uzalishaji wa bidhaa na kusimamia hati miliki kwa wasanii.
Amemalizia kwa kusema kuwa anataka Tanzania katika upande wa afya watu watoke nje kuja Tanzania kupata matibabu kwani wataalamu tunao.