Azam Media imebainisha kutoa bonusi ya Sh 500 milioni kwa misimu mitatu mfululizo kwa bingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara kuanzia msimu ujao wa 2021/2022.

Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Tido Mhando amesema kwenye kila nafasi ya msimamo wa Ligi kutakuwa na bonusi kwa misimu mitatu ijayo.

“Bingwa atapata Sh 500 milioni, wa pili Sh250 milioni, watatu Sh225 milioni, wa nne Sh 200 milioni.

“Kila nafasi kutakuwa na bonusi yake hadi mwisho, timu zote za Ligi mwishoni mwa msimu itapata chochote.

Amesema itakayomaliza ya tano itapata Sh 65 milioni, 60 milioni timu itakayomaliza ya sita na ya saba itapata 55 milioni,  na bonusi hiyo itaendelea kushuka hadi kwenye timu itakayocheza Playoff ambayo itapata bonusi ya Sh 20 milioni

“Bonusi itaongezeka kila msimu katika kipindi cha miaka 10, lengo ni kuhakikisha klabu zinasafiri vizuri, zinalipa wachezaji wake na kuweza kusafiri,”

Ajira za walimu gumzo Bungeni
Jaribio la mapinduzi Mali: Rais, Waziri Mkuu washikiliwa na Jeshi