Aliyekua beki kisiki wa Manchester United Nemanja Vidic huenda akarejea England lakini safari hii ni kujiunga na Aston Villa kama mchezaji huru.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 34, ameachana na Inter Milan baada ya kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na sasa timu yoyote itakayomchukua, itamzoa bure bila ada ya uhamisho.

Villa inaongoza mbio za kumnasa beki huyo lakini inataka kujiridhisha kuwa  yupo fiti kutokana na ukweli kuwa mechi yake ya mwisho ya kimashindano ilikuwa mwezi Mei mwaka jana dhidi ya Juventus.

Arsene Wenger Avunja Ukimya Kuhusu Game Ya Stoke City
Taarifa Kuhusu Kusimamishwa Kwa Viongozi Wa TEFA