Alioyekua beki Manchester United, Nemanja Vidic ambaye amevunja ukimya na kukiri anarejea katika Ligi Kuu ya England.

Beki huyo amesema amevunja mkataba wake na klabu ya Inter Milan na hiyo haina maana kwamba maisha yake ya kisoka yamefikia kikomo bali anatazama changamoto nyingine na kusema wazi kwamba anataka kurejea katika Ligi Kuu ya Uingereza yenye msisimko mkubwa.

Klabu ya Aston Villa imehusishwa kwamba inataka kumsaini Vidic kama mchezaji huru bada ya nyota huyo wa zamani wa Manchester United kuvunja mktataba wa klabu yake ya Inter Milan inayoshiriki Ligi Kuu ya soka ya serie A nchini Italia.

Lakini pia Vidic mwenye umri wa miaka 34, anahusishwa kutimkia kucheza soka nchini Marekani kwenye Ligi ya MLS lakini pia huenda akarejea nchini England kukipiga kwenye Ligi Kuu ya nchi hiyo.

Aston Villa wamekuwa wakipambana kusaka kiongozi atakayeiongoza safu yao ya ulinzi, mbali ya Vidic pia Villa wanaifukuzia saini ya mlinzi wa kati wa Bordeaux, Lamine Sane.

Joe Lescott huenda akatimkia China huku pia kukiwa na taarifa beki huyo wa zamani wa Man City anaweza akajiunga na klabu ya LA Galax ya Marekani.

Nemanja Vidic ambaye ni raia kutoka nchini Serbia, ameiacha klabu ya soka ya Inter Milan ya nchini Italia baada ya mkataba wake kusitishwa kwa makubaliano maalum mapema wiki iliyopita.

Nahodha huyo wa zamani wa Manchester United alijiungana klabu hiyo ya Inter Milan mwezi Julai, 2014 na kuichezea mechi 28 tu katika msimu wa mwaka jana, lakini akashindwa kucheza tangu kuanza kwa msimu huu kutokana na kutingwa na majeruhi.

“Klabu ya Internazionale wangependa kutangaza kwamba klabu inavunja mkataba na Nemanja Vidic baada ya maridhiano malum,” Inter iliandika katika tovuti yake. Vidic ambaye pamoja na mlinzi mwenzie, Rio Ferdinand walitengeneza ngome isiyo na kifani nchini England na Ulaya kwa ujumla na kuisaidia klabu ya Manchester United kutwaa mataji mbalimbali ikiwemo pia Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2008, ameishukuru klabu ya Inter na mashabiki wake.

“Napenda kuwatakia mafanikio makubwa zaidi kama klabu katika siku zijazo,” alimalizia Vidic.

Jurgen Klopp Awatuliza Mashabiki Wa Liverpool
Zitto aunga mkono Magufuli kumkamata Mmiliki wa IPTL aliyezalisha Sakata la Escrow